Jamii zetu za Kitanzania, mara nyingi sana ni za watu wa matabaka matatu tofauti, yaani zile zinazo ishi maisha ya kawaida na za pili ni zile ambazo zinaishi maisha ya shida sana yaani ya kimaskini chini ya dola moja ya kimarekani kwa siku moja. Na kundi la tatu ni hili linaloishi maisha ya kitajiri yaani linatumia hadi dola 10 kwa siku na kuwa na sehemu nzuri ya kujihifadhi na pia kujilimbikizia mali nyingi kwa ajili ya wakati ujao.
Hebu tuangalie haya makundi katika jamii.
Wakati mwalimu nyereren alipoikomboa nchi hii lengo lake kuu lilikuwa ni kujenga nchi ya ujamaa na kujitegemea, ndio maana kukawa na mabo mengi kama uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa katika baadhi ya miji hapa nchini.
Lakini sasa ujamaa umekufa, hatuwezi kujiita watanzania wote, wapo watanzania naupa watanganyika bado. Kwani wapo ambao wanaweza kula na kutupa chakula,kwenye pipa la taka lakini wapo ambao hata mlo mmoja unakosekana kwa siku. Kwanini mwingine apate na mwingine akose? je hali hii inaeleza kwamba wapo wenye akili sana zaidi ya wengine?
Hebu tuone kuwa hapa Tanzania ili uweze kuwa na kazi nzuri na kuishi maisha mazuri ni lazima uwe na elimu ya kutosha na kuwa na ujuzi fulani utakao kupatia kipato kidogo cha kujikimu. Wapo ambao wanafanya kazi kubwa sana na wanavuja jasho sana, lakini bado utakuta wanaishi maisha ya shida sana hata kuliko wale ambao wanafanya kazi za kawaida. Jambo hili linaweza kuifanya hii jamii ya kitanzania ilio kwenye kazi ngumu na kuacha kufanya kazi hizo na kujiingiza kwenye kazi nyingine. Mfano mkulima wa kawaida, yeye na jembe jembe na yeye halafu inafika wakati wa mavuno, wanunuzi wanakuja na kununua kwa bei rahisi bila kujua kuwa huyu bwana alitumia nguvu sana katika kuandaa shamba pamoja na kupata mbegu pamoja na kilimo.Ndugu zangu hebu tujadiliane kujua kuwa ni jambo gani hasa lifanyike ili kweza kuisaidia jamii hii?
No comments:
Post a Comment