Wednesday, February 20, 2013


St. Peter The First Pope of Catholic Church.
32--67. B.C
Baba Mtakatifu wa Kwanza kabisa ni Mt. Petro ambaye ndiye Mwanzilishi na Halifa wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristu. Habari zake Nyingi zimeandikwa katika Biblia Takatifu  Agano Jipya. Pia wakati wa kukabidhiwa madaraka na Bwana Yesu Kristu Mwenyewe alimweleza kuchunga kondoo wake na Pia alimtabiria habari za Kifo chake ( Yohana 21:18)

Na aliongoza Kanisa katoliki Toka Mwaka wa 32 hadi Mwaka wa 67. alipouwawa kwa kusulibiwa katika Msalaba . katika kifo chake Petro alipoona Msalaba, alikataa kusulibiwa kama Yesu ambaye ni Mwokozi ila akawaambia wamsulibishe  kichwa  chini miguu juu, ili asijifananishe na Mwokozi. Ndivyo ilivyokuwa Mwisho wa Petro na nafasi yake ikachukuliwa na Baba Mtakatifu Linus kutoka Mwaka huo wa 67

No comments:

Post a Comment