Wednesday, February 20, 2013

St. Linus 2nd Pope 67-76
Baba Mtakatifu Linus ni Papa aliyemfuata Mtakatifu Petro baada ya kifo chake na aliongoza toka Mwaka 67-76 na huyu Ndiye anayetajwa katika Agano jipya kama Mt. Petro kama ilivyo kwa Petro Mt. Linus aliliongoza kanisa katika mazingira Magumu na alikuwa pamoja na Petro enzi hizo za utawala wa Roma. watu waliweza kumwita Petro wa pili kulingana na jinsi alivyokuwa anapenda kufanya kazi kwa ujasiri mkubwa katika mazingira magumu. alifariki Mwaka wa 76 B C na nafasi yake kuchukuliwa na  Baba Mtakatifu St. Anacletus Mwaka huo huo wa 76.

St. Peter The First Pope of Catholic Church.
32--67. B.C
Baba Mtakatifu wa Kwanza kabisa ni Mt. Petro ambaye ndiye Mwanzilishi na Halifa wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristu. Habari zake Nyingi zimeandikwa katika Biblia Takatifu  Agano Jipya. Pia wakati wa kukabidhiwa madaraka na Bwana Yesu Kristu Mwenyewe alimweleza kuchunga kondoo wake na Pia alimtabiria habari za Kifo chake ( Yohana 21:18)

Na aliongoza Kanisa katoliki Toka Mwaka wa 32 hadi Mwaka wa 67. alipouwawa kwa kusulibiwa katika Msalaba . katika kifo chake Petro alipoona Msalaba, alikataa kusulibiwa kama Yesu ambaye ni Mwokozi ila akawaambia wamsulibishe  kichwa  chini miguu juu, ili asijifananishe na Mwokozi. Ndivyo ilivyokuwa Mwisho wa Petro na nafasi yake ikachukuliwa na Baba Mtakatifu Linus kutoka Mwaka huo wa 67

                                        Baba Mtakatifu Benedict XV1 2005---2013

                              KANISA KATOLIKI  LA ROMA NA VIONGOZI WAKE.. 01.
Baba Mtakatifu Benedict XV1 ametangaza kujiuzulu ifikapo tarehe 28 mwezi  february mwaka huu 2013. Hayo yanatokea baada ya kuona kwamba afya yake haimruhusu kuendelea kuongoza kanisa hili kubwa ambalo lina zaidi ya waumini 2m duniani kote.

Benedict ni Papa wa 265 katika orodha ya mapapa wa kanisa Katoliki tangu kuasisiwa kwake na Mt. Petro mwaka wa 32 Baada ya Kristo. Baba Mtakatifu Benedict XV1 aliingia madarakani Mwaka 2005 akichukuwa wadhifa huo baada ya aliyekuwa Baba Mtakatifu  Yohane Paulo 11 kuaga Dunia.

Ni Papa wa Kwanza kutangaza kujiuzulu Baada ya Miaka 600 kwani mara ya Mwisho kutangaza kujiuzulu ilikuwa mwaka 1415 ana aliitwa Papa Gregory X11.

Sasa hapa Nitakuletea kwa ufupi habari za Maaskofu hawa wakuu wa kanisa katoliki Kuanzia Mt. Petro  Mpaka Baba Mtakatifu atakaye fuata Baada ya huyu Benedict wa kumi nasita ambaye ni Baba Mtakatifu wa 265.

Tuesday, January 29, 2013

mama Lenon na Mama Junior wakiwa nyumbani.
david na mama yake wakiwa wamepumzika nyumbani.

Friday, December 28, 2012

 Mama yangu Mzazi akiwa amevaa mavazi ya Shirika la Moyo Mt. wa Yesu ambapo yeye ni Mwanashirika hilo.
 dini ni jambo lingine ambalo tunapswa kulizingatia maana ndilo linatupa Mwanga Bora wa kiimani
                                           MOYO MTAKATIFU WA YESU. UTUHURUMIE.